Tuesday, July 3, 2012

WEWE NI NANI?


Michael anamwona brad akija,na anahofia kitakachotokea. " sema michael,hebu onja kidogo"brad anamwambia michael,brad anapofungua mkono wake anaona kitu alichotegemea kukiona -msokoto wa bange.hataki kuukubali lakini pia hataki kudharauliawa na vijana wenzake. Michael anajibu kwa woga " sio leo labda wakati mwingine?"


“jessica anamwona brad akija, na yupo tayari kwa kitakachotokea "sema jesca hebu onja!" brad anamwambia jessica,jessica anaona kitu alichojua atakiona-msokoto wa bangi. "hapana sitaki" jessica anamjibu kwa ujasiri " nina mpango fulani kwa wakati ujao na hivyo sitaki kuhatarisha afya yangu,pia brad mtu mwenye akili timamu hawezi kuvuta bangi"

Katika mifano miwili hapo juu kati ya michael na brad, halafu jessica na brad tumeona jessica ameweza kukabiliana vizuri na brad kulilo michael,kwa sababu jessica ana kitu ambacho michael hana,Unajua ni nini? Ni KITAMBULISHO,si kitambulisho kama kadi inayoonyesha jina na picha yake. KITAMBULISHO hicho ni hisia ya ndani inayokutambulisha wewe ni nani na unaongozwa na viwango gani.Unapokuwa na kitambisho hicho,unakuwa na nguvu ya kushinda majaribu na hivyo kudhibiti maisha yako badala badala ya kuacha wengine wayadhibiti.Unaweza kukuza uwezo huo jinsi gani? Huenda kwanza inafaa kujibu maswali yafuatayo;



1.     .Nina SIFA GANI NZURI?
Kwa nini ni muhimu kujua una sifa gani?kwa sababu itakufanya kujua uwezo wako, na sifa nzuri kutafanya ujiamini zaidi.


2.     NINA UDHAIFU GANI?
Kwa nini ni muhimu kujua udhaifu wako?
Kama vile ilivyo rahisi kwa mnyororo kukatika ukiwa una kiunganishi fulani dhaifu ,ndivyo hivyo pia utambulisho wako unavyoweza kuharibika ikiwa utaruhusu udhaifu wako udhibiti maisha yako.Kila mmoja wetu ana udhaifu ambao angependa kuushinda,lakini huwezi kuushinda udhaifu wako kama hujaujua udhaifu wako,kaa tafakari udhaifu ulinao hatimaye utajigundua,au mwambie rafiki yako wa karibu unayemwamini akwambie udhaifu wako wote asikufiche kitu chochote NI BORA KUSIKIA MANENO YATAKAYOKUUMIZA LAKINI YENYE UKWELI KULIKO MANENO MATAMU YENYE KUKUDANGANYA .Hakuna binadamu asiye na udhaifu,ila pale unapoujua udhaifu wako ndipo unapoweza kuurekebisha na kujitambua zaidi na kuelekea kwenya mafanikio ,



3.     NINA MRADI GANI?
Kwa nini ni muhimu?
-unapojiwekea mradi maisha yako yanakuwa na mwelekeo na kusudi,pia utaweza kuepuka watu na hali ambazo huenda zikakuzuia kutimiza mambo ambayo umeamua kutimiza
FIKIRIA HILI: je,unaweza kuingia ndani ya teksi na kumwambia dereva wa gari hilo aendeshe akizunguka jengo moja hadi mafuta yaishe? Huo ni ujinga na utakugharimu sana! Miradi humsaidia mtu awe na mwelekeo maishani,unakuwa na mahali pa kwenda na unapanga jinsi ya kifika huko.
JICHUNGUZE. Hapa chini andika miradi mitatu ambayo ungependa kutimiza kufikia mwaka ujao,
1...............................
2................................
3................................
Sasa chagua mradi ambao unaona muhimu zaidi kwako,kisha uandike kike unachoweza kufanya saa hivi ili uweze kuufikia.

4.NINA MSIMAMO GANI?
Kwa nini ni muhimu kujua nina msimamo gani?
- Bila ya kuwa na msimamo gani maamuzi yako hayatakuwa imara.kama tu kinyonga ,utabadili msimamo wako kila mara ili ukubaliwe na vijana wenzako- ishara ya wazi kwamba huna UTAMBULISHO wako mwenyewe,naomba ujichunguze unamsimamo gani?

Je ungependa kufanananishwa na nini?
-JANI linaloangushwa na kupeperushwa na upepo huku na huko au MTI unaohimili hata dhoruba kali? Ukidumisha utambulisho wako ukiwa dhabiti utakuwa kama huo MTI. Na hilo litakusaidia kujibu swali hili. WEWE NI NANI?


Ahsante kwa kutembelea blog hii
tembelea mara nyingi uwezavyo maana itakwenda kukufanya ujitambue
mungu akubariki sana

                                                       

wako mchumi faraja mmasa a.k.a MOA
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.