Thursday, July 18, 2013

Ubongo wa mtoto mchanga umesemwa kuwa ndio mashine yenye uwezo zaidi ulimwenguni,

Ubongo wa mtoto mchanga umesemwa kuwa ndio mashine yenye uwezo zaidi ulimwenguni, na kwa sababu mtoto anazaliwa akiwa tayari kufyonza kila kitu anachoona,kusikia na kugusa.Zaidi ya yote mtoto huvutiwa na wanadamu wengine ,yaani anavutiwa watu wanapomgusa ,anavutiwa na nyuso na sauti zao kitabu cha babyhood kilichoandikwa na penelope leach kinasema hivi  “uchunguzi   umefanywa kuhusu mambo yanayovutia zaidi macho ya mtoto ,sauti zinazovutia  fikira zake na vitu anavyopenda kugusa mara nyingi yote hayo hutimizwa kwa urahisi na mtu mzima anayemtunza.Haishangazi kwamba wazazi wanatimiza fungu muhimu katika ukuzi wa mtoto.Wazazi na vile vile madaktari wa watoto wanashangzwa sana na uwezo wa mtoto wa kujifunza lugha kwa kusikia tu.




Watafiti wamegundua kwamba siku chache tu baada ya kuzaliwa mtoto anajua sauti ya mama yake  na anaipenda kuliko sauti ya mtu asiyemfahamu,majuma machache tu baadae mtoto anaweza kutofautisha kati ya sauti ya lugha ya wazazi wake na lugha nyingine na miezi michache baadae anaweza kutofautisha kati ya maneno na hivyo anaweza kutofautisha usemi wa kawaida na sauti zisizoweza kueleweka.Mtoto mchanga husema kwa njia gani?kwa kawaida anabubujika kwa mambo yasiyoeleweka .Je hizo ni kelele zisizo na maana ? la! Katika kitabu chake whats is going on in there? How the brain and mind develop in the first five years of life.Lise Eliot anatukumbusha kwamba “ingawa huenda ikaonekana kwamba kusudi la sauti zisizoeleweka za watoto wachanga ni kuvuta fikira za watu tu,sauti hizo hutimiza jambo muhimu katika kuzoeza misuli kusonga kwa upatano wa kati atakapoanza kuongea,wazazi wanapoongea kwa msisimuko mwingi pamoja na watoto  wao mchanga anapopiga kelele zisizoeleweka ,ilo hutimiza kusudi fulani,msisimuko huo humchochea mtoto aendelee kutokeza sauti hizo,mazungumzo hayo kati ya mtoto na mzazi humfundisha mtoto mchanga mambo yanayohusika katika mazungumzo-ustadi ambao atautumia katika maisha yake yote.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.