Monday, August 19, 2013

MBINU 20 KWA MWANAFUZI/MWANACHUO KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO YAKE- PART 2



Karibu katika blog ya FARAJA MMASA BLOG,naamini ni mzima wa afya njema,mungu aliyetuumba anaendelea kutupigania kwa namna moja au nyingine,leo naendelea sehemu ya pili (part 2) ya somo la mbinu 20 za mafanikio katika masomo,ni somo zuri kwa wanafunzi na wanchuo ili kuweza kujipatia mafanikio katika masomo yao na maisha yao kwa ujumla,kama hujasoma sehemu ya kwanza basi unaweza kubonyeza hii link Katika somo la leo nitajikita zaidi katika utunzaji wa kumbukumbu,ambalo ni jambo muhimu zaidi kwa mwanafunzi MBINU 2O KWA MWANACHUO/MWANAFUNZI KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1 ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yake.Uchunguzi unaonyesha kuwa watu ambao huzingatia suala la kanuni za afya zikiwemo mbinu za kutunza kumbukumbu ya akili hupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa seli zinazojenga uwezo wa akili katika kutunza kumbukumbu(suzan tapert mwanasaikolojia kutoka Chuo cha Califonia san Diego nchini Marekani anathibitisha haya pia) ili mwanafunzi aweze kutunza na kujiongezea kumbukumbu zake basi inampasa kuyafanya haya yafuatayo


     6.LISHE BORA
Ni wazi kuwa watu wengi tunafahamu maana ya lishe bora,lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo cha American Acedamy of Neurology kinachojihususha na mambo ya neva ,ulibaini kuwa machungwa,spinachi,karoti,mogamboga,viazi vitamu huuongezea uhai ubongo na kufanya mwanadamu asiweze kushambuliwa na magonjwa ya kupooza.

Aidha matunda na vyakula vyenye vitamini b,folik acid (folic acid) ,niasin (niacin) kalkamin( curcumin) husaidia kufanya ubongo uwe na mawasiliano ya kutosha na viungo vingine vya mwili na kupunguza kwa asilimia 11 uhalibifu wa seli ndani ubongo.Utafiti wan National Reseach Council Nchin Milan,Italy unathibitisha kuwa vyakula vyenye vitamin E hupunguza kiwango cha usahaulifu.

7.MAZOEZI YA MWILI
Ufanyaji wa mazoezi ya mwili huimarisha misuli na kusaidia akili kuweza kufanya kazi vema,hii inatokana na ukweli kwamba tunapofanya mazoezi tunakuwa  tunaongeza msukumo msukumo wa damu mwilini na hivyo kuufanya ubongo kufikiwa na damu ya kutosha ambayo ni muhimu kwa uimara wa kumbukumbu.mara nyingi mazoezi yanayofaa zaidi kwa afya ya mwili na uimarishaji ni yale ya asubuhi na jioni. Kuhusu aina ya mazoezi inategemea na umbo la mtu lakini kukimbia kuruka kamba,kucheza mpira ni bora kwa afya..Mazoezi ya aina hii yakifanywa  na Wanafunzi huwasaidia pia kutunza utunzaji wa kumbukumbu  za masomo wanayofundishwa.


 8.UTUMIAJI WA VINYWAJI

Vinywaji kama kahawa,chai nyeusi navyo huchangia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu,inashauriwa kwa mwanadamu kutumia walau  kikombe kimoja cha vinywaji hivyo ili kuongeza enzymes ambazo ni muhimu  kwa kuongeza nguvu ubongo ili kuweza kutunza kumbukumbu,hata hivyo vinywaji vikali kama pombe havirusiwi  kwani huchangia kudumaza uwezo wa kumbukumbu.
Baada ya kuangalia mambo muhimu katika utunzaji wa kumbukumbu,basi tuendelee na mbinu nyingine ambazo pia ni muhimu ili uweze kupata mafanikio katika masomo yako

9.UNAPOKUWA DARASANI MSIKILIZE MWALIMU KWA UMAKINI MKUBWA
Wanafunzi wengi wanapokuwa darasani hasa katika hichi kizazi cha mtandao wanakosa umakini katika kumsikiliza mwalimu ,pale anapokuwa anafundisha.Hakikisha mwalimu anapokuwa anafundisha unaweza kumsikiliza kwa umakini huku ukiwa na NOTEBOOK ili kuweza kuandika vile vitu muhimu ambavyo vitakuwa na msaada katika siku za mbeleni,hakisha pale unaposhindwa kuelewa unanyoosha mkono na kumuuliza mwalimu kwa kile usichoelewa ingawa katika shule zenu nyingi hasa za kayumba utaonekana unajishaua sana,ndugu yangu angalia nini unahitaji na sio watu watasema nini juu yako shuleni ulienda peke yako na ipo siku utaondoka peke yako,hakikisha unaondoka na ulichofuata. Swala la msingi hapa unapokuwa darasani kufunga ubungo wako katika maswala yote na kubaki kumsikiliza mwalimu tu,kama ni mwanachuo zima simu yako au weka silent kwenye begi mpaka utakapotoka  ili usiweze kuhamisha akili yako sehemu nyingine kwa mfano pale itakapoingia mesegi,hakikisha kila kipindi kikiisha umeingiza kitu kipya ambacho ulikuwa hukijui hapo kabla.
10.JIANDAE KWA KILA KITU KABLA HUJAANZA KUJISOMEA BINAFSI
Ni lazima kwa kila mwanafunzi kuwa na muda maalam wa kujisomea yeye mwenyewe binafsi ukiacha na ule muda wa jadiliana katika makundi mbalimbali,hakikisha kabla hujaanza kusoma umeandaa kila kitu cha msingi unachotakiwa kuwa nacho ,kama unasoma hesabu basi hakikisha vitu vyote vinavyohusiana na somo la hisabati,kama  ni calculator,penseli,mkebe ,past papers,vitabu ,sio unasoma mara umesahau kitu kipo kwa rafiki yako kwa hiyo ufunge tena safari,au umeshau chumbani,hii itakufanya ukose utulivu ,jua kabisa leo nina ratiba ya somo Fulani kwa hiyo fanya maandaliza toka mapema,pia hakikisha unasaa pembeni ili ujue kabisa muda unaotumia katika kusoma,kama ni masaa mawili basi ujue ni masaa mawili,maana unaweza kuwa umetumia nusu saa tu ndio uliyotulia na kusoma muda wote ulitumia katika kutembea tembea
Usikose sehemu ya tatu ya mada hii hapa
Wako faraja mmasa a.k.a moa
Kama hujasoma sehemu ya kwanza ya mada hii bonyeza hii link hapa
MBINU 20 KWA MWANAFUNZI?MWANACHUO KUPATA MAFANIKIO KWENYE MASOMO-PART 1
Pia nakuomba usikose kusoma kitabu changu kiatakapotoka ambacho kitakufanya upate uelewa wa mambo mengi

***************DUNIANI TUNAPITA USIACHE KUTENDA MEMA,JUA IPO SIKU UTAIACHA HII DUNIA,WAKTI MWINGINE KABLA HUJALA JIULIZE KAMA KESHO HUTAIONA UTAIWEKA WAPI ROHO YAKO BAADA YA MAISHA YA KIDUNIA***************************************
Share:

Healing after a Divorce or Breakup




Healing after a Divorce or Breakup

Why do breakups hurt so much, even when the relationship is no longer good? A divorce or breakup is painful because it represents the loss, not just of the relationship, but also of shared dreams and commitments. Romantic relationships begin on a high note of excitement and hope for the future. When these relationships fail, we experience profound disappointment, stress, and grief.
Share:

UNAJUA ZAWADI MAALUMU YA KUMPA MWANAO ATAKAYOIKUMBUKA NA KUMSAIDIA MAISHA YAKE YOTE? HIZI NDIZO ZAWADII ZA KUMPA MWANAO





Tumezoea kuwanunulia watoto wetu zawadi mbalimbali hasa katika siku muhimu kama kumbukumbu ya kuzaliwa. Mara nyingi zawadi hizo wanazifurahia sana wanapozipata na baada ya muda mfupi wanapoteza hamu nazo. Kuna zawadi za muhimu sana kwa mtoto wako na atakuwa nazo mwaka mzima na kuzifurahia siku zote.

1. Zawadi ya Upendo
Muonyeshe mtoto wako kuwa unampenda kwa maneno na vitendo. Mkumbatie mara kwa mara hasa wakati akiwa na huzuni au hofu na umwambie ni jinsi gani unampenda na unashukuru Mungu kuwa naye kama mtoto wako.

2. Zawadi ya Maonyo
Unapoacha kumuonya mtoto pale anapokosea unakuwa unachangia katika kuyaharibu maisha yake. Mfundishe mtoto utii kwa wazazi na watu wote na hivyo atakuwa anamtii Mungu, na usiache kumuonya pale anapokosea.

3. Zawadi ya Muda
Uwe na muda wa kufurahi na kucheka na mtoto wako. Upatikane kwake pale anapokuhitaji akusimulie hadithi zake, akuulize maswali au tu kupata muda wa kuwa nawewe. Umpe muda wako bila masharti yoyote na awe huru kuwa na wewe bila kujisikia vibaya.

4. Zawadi ya Ukarimu
Mtoto anapofikia umri wa kuanza shule na kujenga marafiki kuna wakati atakuwa anakuja nao nyumbani. Mwonyeshe zawadi ya ukarimu kwa kuwakarimu marafiki zake na kutaka kuwafahamu zaidi
wako faraja mmasa a.k.a moa
 nakuomba usikose kitabu changu pale kitakapotoka
 
Share:

MOURINHO AANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND...CHELSEA YAUA 2-0



KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesherehekea kurejea kwake Stamford Bridge kwa kuanza na ushindi wa mabao 2-0 katika Ligi Kuu ya England dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu, Hull.
Kiasi cha miaka sita tangu aachane The Blues, kocha huyo maarufu kama Special One alifurahia mapokenzi mazuri na mchezo mzuri wa timu yake akirejea nyumbani.
Haikuwa kazi rahisi kwa Chelsea kushinda, baada ya mkwaju wa penalti wa Frank Lampard dakika ya sita kuokolewa na Allan McGregor na sheria ya teknolojia kwenye mstari wa goli ikachukua nafasi yake wakati kipa huyo wa Scotland alipookoa mpira wa kichwa wa Branislav Ivanovic na kudhaniwa ni bao dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, ikisahihisha si bao.
Pamoja na hayo, Chelsea ilipata mabao yake yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Oscar dakika ya 13 na Lampard dakika ya 25.
Kikosi cha Chelsea leo kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Lampard, Ramires, De Bruyne/Schurrle dk67, Oscar/van Ginkel dk85, Hazard, Torres na Lukaku dk75.
Share:

BARCELONA YATOA KIPIGO CHA PAKA MWIZI, YAIGONGA LEVANTE 7-0




Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Alexis Sanchez dakika ya tatu.

Lionel Messi kama kawaida yake katupia mbili katika mechi ya leo.

Neymar aliyeingia kipindi cha pili akikwaana na mchezaji wa Levante.
Share:

UNDER 30 YOUTH AWARDS: JOKATE, MILLARD AYO, BEN POL NA WENGINE WAIBUKA KIDEDEA



Tuzo za vijana walio chini ya umri wa miaka 30, zimetolewa jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia vijana nane wakiibuka washindi kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo Mchango kwenye jamii, Ujasiriamani, Uvumbuzi, Michezo, Burudani, Mitindo na zingine.

Tuzo kubwa ya siku ya Mchango kwenye Jamii (Social Impact) imechukuliwa na Adam Anthony ambaye ni mkurugenzi wa DAELIT Group anayejihusisha na masuala ya mazingira.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.