Thursday, November 14, 2013

World's Richest Dinner Party........!!!


The heads of Apple, Google, Yahoo!, Facebook, Twitter.... oh and the US president.... too......!!!!
From the left 2 right: Eric Schmidt, Arther D levinson, Jhon Doerr, Larry Ellison, Reed Hastings, John Hennessy, Carol Bartz, Dick Costolo, Mark Zuckerberg, Barack Obama, Steve Jobs, Steve Westly, Ann Doerr........!!!
Share:

MBINU ZA BIASHARA







JIBU LA KWA NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa ,nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Share:

Kabichi, faida lukuki kiuchumi na kiafya



Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo


Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.


Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).



Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.



Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.


Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.


Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima. Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja.  Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.


Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche. Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.