Monday, March 31, 2014

ACHA KUONA AIBU WAKATI AIBU HAIONEKANI

Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii,natumaini we ni mzima wa afya  njema mungu anaendelea kukupigania kila siku na kukulinda,hatuna budi sifa na shukrani ni kumrudishia mwenyezi mungu aliyetuumba na kutufikisha hapa leo. Siku ya leo nataka kuongelea mada hii kwa ufupi tu maana wengi wetu tunaona ni jambo dogo lakini wengi wetu huwa linatufanyya tunashindwa kufikia malengo mengi sana katika maisha yetu.

Mara nyingi huwa tunashindwa kutumia fursa zilizopo kwa kuangalia watu watatuchukulia vipi kwa kile ambacho tunakifanya ,kisa tunaona aibu,tuliosoma tupo tayari kufanya kazi za kulipwa laki mbili kwa mwezi lakin zipo kazi za kawaida ambazo mtu anawea kupata hata milioni lakini hatutaki kwa vile tunaona aibu ,utaona aibu mpaka lini? umri unazidi kwenda ,acha kuanagalia watu watakuchukulia vipi? kama huvunji sheria wala maadili unaogopa nini kufanya au kutumia fursa?hata kama haiendani na elimu uliyonayo ,lakini inakuwa ni kwa muda tu kwasababu unakuwa na mipango ya muda mrefu ambayo utafanya inayoendana na hadhi yako,je nikweli ni bora kukaa huna shilingi 5000 au kufanya kazi za kawaida kabisa na kupata shilingi elfu kumi kwa siku? hivi unajua kuna watu mabilionea lakini walifanya sgughuli za kawaida kabisa? je wewe unaogopa nini? acha kuona aibu,hebu fanya hao wanaokucheka siku waje kuwa ndio mawakala wako wa kuhadithia watu kuhusu historia yako.

Watu wengine huona aibu katika kujaribu kwa vile wanaogopa wakishindwa watu watawasema vibaya na kuwacheka,ngoja nikwambie ndugu msomaji mafanikio ni maendeleo ya matokeo ya kushindwa ,kila unaposhindwa basi unakuwa unagundua kitu kitakachokusaidia kusonga mbele,mimi kama faraja siogopi kujaribu na siji kukata tamaa mpaka siku nafukiwa makaburini kwetu misheni gairo lakini hivi na pumzi na ni mzima wa afya nitatumia kila fursa itakyokuja mbele yangu baada ya kuifanyia utafiti wa kutosha ,mimi ni mimi sina ubia kwenye maisha yangu na hata wewe ni wewe huna ubia na yoyote yule .Ngoja nikutajie watu maarufu duniani waliojaribu mara nyingi na kushindwa lakini hawakukata tamaa,wewe unaona aibu kwasababu unaona aibu ukishindwa watakucheka.

Thomas Edson
Huyu ni moja ya wagunduzi wakubwa duniani ,ambaye amegundua vitu vingi sana duniani,kimojawapo ni taa ya umeme hiyo unayoiona inawaka chumbani kwako au sebleni kwako au hapo ofisini kwako ulipo,bwana Thomas Edson alikaa siku moja akiangalia taa ya mafuta ya taa inawaka, wazo likamjia hivi haiwezekani kukaa na taa inayotumia umeme,ndio ukawa mwanzo wa ugunduzi wa taa inayotumia umeme,lakini haikuwa kazi nyepesi alifanya majaribio zaidi  ya 1000 ikashindikana kutokana na historia yake yeye mwenyewe mara ya 1010 ndio taa ya kutumia umeme ikawaka! tena ilimchukua zaidi ya miaka kumi kazi hiyo kukamilika,je wewe ndugu msomaji umejaribu mara ngapi kwa hicho unachokifanya? acha kuogopa  watu wataongea nini juu yako kwa hicho unachokifanya.
Thomas A edson


Carlos slim
Huyu ni mmoja wa matajiri kumi duniani ,mara nyingi ameshaingia katika tatu bora,historia yake ni ndefu ila kwa ufupi tu wakati anaanza kutafuta maisha alishawahi kuuza vitafunwa katika stendi ya treni,je wewe unaogopa nini ,aibu ya nini? kuwa na malengo ya muda mfupi na muda mrefu,unaweza kufanya hicho cha muda mfupi ili baadae kije kukufikisha  katika malengo yako ya muda mrefu,amini katika unachokifanya kifanye katika bidii isiyo ya kawaida.
Carlos slim
Itaendelea…..

Wako faraja mmasa a.k.a MOA.

* SELF FULFILLING PROPHECY*


************Tafuta mafanikio kama utaishi milele lakini kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema kama leo ndio siku yako ya mwisho kuwepo katika dunia hii*****************************


Share:

0 comments:

Post a Comment

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.