Tuesday, February 11, 2014

TUNATAKIWA KUSONGA MBELE KWENYE MAISHA,PAMOJA NA CHANGAMOTO ZINAZOTUKABILI



Nikiwa mdogo nilinyanyaswa kijinsia na kimapenzi na mjomba wangu pamoja na kupigwa sana na bibi yangu huku nikifanyishwa kazinyingi.Nilipigwa mpaka damu zilinitoka mgongoni na kuangukia nguo yangu ya kanisani na baada yabibi kuona hivyo akaanza kunipiga tena tukielekea kanisani huku akiniuliza kwa nini nguo ilikuwa na damu. Nilikula na kunywa maji kwa taabu nilitumia mikono yangu na bibi hakupenda kuniona hivyo akazidi kunichapa.Kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka 6 na nilipofika miaka 9 nilihama kwa bibi na kwendakuishi na mama. Nikiwa na miaka hiyo 9 nikabakwa na mjombawangu baada ya kubakwa damu zikiwa zinachuruzika magotini akanichukua nakunipeleka kuninunulia ice cream. Na niliendelea kuibighudhiwa kimapenzi pamoja na kuendelea kubakwa kuanzia miaka 10 mpaka 14 kabla ya kupata mimba na mama kunifukuza.Nikahamia kwa baba ambaye alinikataza nisijihusishe na mapenzi au kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa aina yoyote ile bila kujua tayari nilikuwa mjamzito.







Wiki mbili baada ya mtoto kuzaliwaalikufa.Ilikuwa huzuni kwangu na kwa baba piaingawa kwangu niliona ni kama nafasi ya pili kwamimi kuanza maisha mapya nikijipanga upya. Maisha ya yule mtoto aliyekufa yalinipa uchungu wa kuona kuwa nahitaji kuyazika yote ya kale na changamoto za utoto hata kama nitakutana na mpya ila mtoto alinipa hamasa ya kujituma na kumtegemea Mungu.Nafahamu ilivyo shida na ngumu kuishi na watu wasio kuthamini au hata kukujali maishani, lakini pia waweza kuutumia mwanya huo kama kichocheo cha mafanikio.Watu wengi tunayaona maisha na changamotozake kama ni kero kwetu na tunaonewa. Una kila sababu ya kusimama na kuzikabili changamotozako. Niliishi katika jamii ambayo mtoto alionekana nahakuthaminiwa na kamwe sikujua kama ndani yangu nilikuwa na nguvu ya kujiamini na kujakufanya mambo makubwa kama haya. Kila mtu ana hadithi tofauti na yenye kukuliza nakukuumiza kuliko hii ya Opra winfrey, lakini hadithi yake ilimfanya ajitambue na kufikia hatuaaliyonayo sasa ya kuwa mwanamke tajiri zaidi duniani. Kupitia hadithi hii tunajifunza kuwa katikamaisha tunatakiwa kusonga mbele pamoja na changamoto mbalimbalu na mwisho tuje kuwa na mwisho mzuri.

 Sala yangu kwako

 Pamoja na mapito magumu nakuombea kwa mwenyezi Mungu kila changamoto uipitiayo sasa ije kugeuka na kuwa mafanikio yako kwa kadri utakavyo mtanguliza Mungu katika mapito yako huku ukijituma. Na utafanikiwa na kuja kuwa mfano kwa jamii yako...



Amen credit:dunia ni chumba cha mitihani.
wako faraja mmasa

***** tafuta mafanikio kama utaishi milele,lakini kumbuka kumcha mungu kama leo ndio siku yako ya mwisho duniani*****************
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.