Habari za leo unayesoma blog hii,natumainI
wewe ni mzima wa afya njema,mungu anazidi kukupigania kila siku.Nimekuwa siku
nyingi nikihaidi kutoa elimu kuhusu hisa
,leo basi naanza kuelezea kwa undani kuhusu somo la HISA.Naamini mpaka mwisho
wa somo hili utakuwa umepata ujasiri wa kuwekeza kwenye SOKO LA HISA,mimi
nimeanza kidogo sasa ,lengo langu baada ya miaka kumi niwe nimewekeza kwa
kiwango kikubwa na kuchuma faida kubwa.
Hisa ni mali.Hisa ni rasilimali.Hisa ni kitega uchumi kinachoweza kukupa fedha.Hisa ni hatimiliki ya kampuni.Hisa ni biashara.Hisa hukuwezesha kupata fedha kupitia mikopo,Hisa hukufanya kupata nguvu ya maamuzi.Hisa ni mtaji.kumiliki UCHUMI na FAIDA kupitia makampuni,hutegemea umiliki wa hisa.HISA SIYO KIPANDE CHA MSINGI BALI NI HAZINA.
Hisa ni kumiliki kampuni,ukitaka kumiliki kampuni ,nunua na umiliki hisa zake,kama vile hati ya kumiliki ardhi (title deed) inavyoonyesha ushahidi wa kumiliki ardhi ;kadhalika cheti cha hisa ( share certificate) kinathibitisha umiliki wa kampuni wa biashara.Kiwango cha umiliki wa kampuni hutegemea idadi ya hisa anazomiliki mwanahisa.kumiliki hisa ni kuwekeza kwenye kampuni,kama unamiliki hisa nyingi,zaidi ya asilimia 50%,basi unakuwa na nafasi kubwa ya kufanya uamuzi katika kampuni inayohusika.
Kampuni inaweza kupata kama mtaji wa kununua rasilimali,mitambo,mashine,kuendesha biashara na kwa kuuuza hisa zake,hivyo hisa zinazouzwa zinaleta fedha kwa kampuni kama mtaji wa biashara.Ukinunua hisa unatoa fedha na ukiuza hisa unapata fedha. Hisa humpatia mwanahisa faida kwa njia ya gawio,ongezeko la thamani,mkopo na kadhalika,nitaelezea zaidi mada za mbele. Kama kampuni ina mtaji wa shilingi laki moja na wewe umenunua hisa za shilingi elfu hamsini, maana yake utakuwa na nguvu ya kushiriki hata kwenye maamuzi nyeti yahusuyo kampuni au biashara husika, tofauti na mtu mwenye hisa za kwa mfano shilini elfu kumi.
Mtu akisema nina hisa NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.
Hisa ni mali iliyorahisi kubadilishwa na kuwa
fedha taslimu kama vile ardhi,nyumba,mitambo na mashine ni mali kwa kuwa zina
thamani,hisa ni rahisi zaidi kuibadilisha na kuwa na fedha taslimu. Faida ya
kampuni ni mali ya wanahisa.Ukimiliki hisa unamiliki mali za kampuni pamoja na
faida.
Hisa ni aina mojawapo ya kuhifadhi fedha
katika mfumo wa akiba.Fedha inayowekwa akiba inaweza kutumika kwa ajili ya kununua hisa na hivyo kubadilisha
muundo wa akiba kutoka fedha taslimu na kuwa katika muundo wa hisa.
Mada hii inaendela,usiache kuifuatilia mpaka
mwisho.…..
Wako faraja mmasa a.k.a MOA
***************Tafuta kupata mafanikio kama utaishi milele
lakini kumbuka kumcha Mungu wako na kutenda mema kama leo ndio siku yako ya
mwisho kuwepo katika Dunia hii*************