Wednesday, February 26, 2014

MASWALI 20 MUHIMU YA KUJIULIZA KABLA YA KUANZA BIASHARA




Habari za leo msomaji wa FARAJA MMASA BLOG,natumaini umzima wa afya njema mungu anaendelea kukupigania.leo naandika kuhusu mambo muhimu  ya kujiuliza kabla ya kuanza biashara,wengi wetu tumekuwa tukianza biashara kwa kukurupuka bila kwanza kufanya utafiti wa biashara tunayotaka kufanya na kupata taarifa za kutosha,matokeo yake tunajikuta katika wakati mbaya ,kabla hujafanya au wakati unafanya utafiti wa biashara unayotaka uifanya hebu jiulize maswali haya kwanza


1.         Kwanini nataka kuanza biashara?
2.         Ni aina gani ya biashara ninayoitaka?
3.         Wateja wangu watakuwa wa aina gani?
4.         Nitauza bidhaa au hudama ya aina gani?
5.         Tayari nimejiandaa kutumia muda wangu na pesa kufanya biashara ianze?

6.         Biashara yangu itakuwa sehemu gani?
7.         Watakaokuwa wananiuzia malighafi ni kina nani au bidhaa nitakuwa nanua wapi ?
8.         Ninahitaji wafanyakazi wangapi?
9.         Ninahitaji pesa kiasi gani ili niweze kuanzisha biashara yangu?
10.       Je ninahitaji mkopo?
11.       Itanichukua muda gani mpaka niweze kuanza biashara yangu?
12.       Ninahitaji mkopo?
13.       Itanichukua muda gani mpaka kuanza kutengeneza faida inayoridhisha?
14.       Nani ni washindani wangu wakubwa?
15.       Bei ya bidhaa au huduma yangu itakuwa vipi kulinganisha na washindani wangu?
16.       Nitauweka vipi mfumo wa kisheria wa biashara yangu?
17.       Nitalipa kodi kwa kiwango gani?
18.       Ninahitaji bima ya aina gani?
19.       Nitaingoza vipi biashara yangu?
20.       Je nitaitangaza vipi biashara yangu kuweza kujulikana kwa watu?
Share:

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE MABWAWA




            

Bwawa la maji
Wakulima wanaweza kuongeza kipato kutokana na ufugaji wa samaki katika maeneo yao
Ufugaji wa samaki kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Mbali na hilo, mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla ya kuanza ufugaji. Moja ya vigezo hivyo ni soko. Si jambo la busara kuanza shughuli yoyote kabla haujafanya uchunguzi na kujua kama kuna mahitaji ya bidhaa unayokusudia kuzalisha. Wafugaji wengi wameanzisha ufugaji wa samaki lakini wakaishia kupata hasara kutokana na ukosefu wa soko. Na wengine wameanguka kutokana na utunzaji mbovu wa mabwawa ya samaki.

Maji
 Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki. Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji. Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki. Wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatika yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Kwa wakazi wa Dar es
Salaam, inawezekana pia kufuga samaki kwenye bwawa, endapo maji yana chumvi ya wastani, na kwa kiwango kinachoshauriwa kitaalamu, basi samaki wanaweza kustahimili, na kukua vizuri
.

Bwawa

Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.

Utengenezaji wa bwawa la samaki kwa maeneo yenye udongo wa kichanga kama Dar es Salaam, mfugaji atalazimika kuchimba na kuweka karatasi ya nailoni. Hii, itasaidia kuzuia upotevu wa maji pamoja na kuzuia bwawa kuporomoka.

Ni vyema upande mmoja wa bwawa ukawa na kina kirefu kuliko mwingine. Upande mmoja unaweza kuwa na kina cha mita moja na nusu, na mwingine mita moja. Hii itamsaidia mfugaji kuweza kulihudumia bwawa vizuri, hata kama ni kuingia na kufanya usafi.

Utunzaji wa bwawa

Samaki 1Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara, hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.

Ulishaji

Wafugaji walio wengi, wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishaji wa samaki. Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha samaki mara mbili hadi mara tatu kwa siku.

Aina ya chakula

Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa. Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi, bali kiwe mabonge madogo madogo, kwa wastani wa tambi.

Magonjwa

Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia, ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu (fangasi), magonjwa yatokanayo na virusi, pamoja na minyoo.

Samaki wanaposhambuliwa na fangasi, huonekana kwa macho kwa kuwa huwa na madoa madoa. Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege.

Pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwa kuwa huzubaa sehemu moja kwa muda mrefu. Magonjwa kwa samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano kwenye bwawa. Hivyo, ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.

Tiba

Tiba iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji, kasha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa, kisha kuwatoa na
kuwarudisha bwawani.

Upatikanaji

Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki Kingolwira Morogoro. Bei ya kifaranga cha Perege ni shilingi 50, na Kambale ni shilingi 150.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Bwana Kalinga kwa simu namba 0757891 761, 0787 596 798

CREDIT: MKULIMA MBUNIFU
Share:

KUWA NA UTU NI KITU CHA MUHIMU KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU

Picha hii inamwonyesha binti mdogo wa kisudani akiwa ananyemelewa na ndege mla nyama aina ya tai.


Binti huyu alianguka njianibaada ya kushindwa kuhimili njaa kali iliyokiwa imembana na alikuwa akielekea katika kituo cha msaada wa chakula.Tai huyo mla nyama za
viumbe hai alimla mtoto huyo na ndio ukawa mwisho wa uhai wake uliomkuta akiwa njiani kuelekea kuokoa uhai wake.

Picha hii ilipigwa namwandishi wa habari aitwaye Kevin Carter na Kwa mara ya kwanza ilichapishwa kwenye
gazeti tarehe 26 Marchmwaka 1993. Pia na kupitia picha hii Carter alishinda tuzo ya Pulitzer Prize mwaka 1994. Miezi michache baada ya kuchukua zawadi ya Pulitzer, Carter alikutwa akiwa amejiua kwa
kuumia kwa kitendo chakinyama alichokifanya nawatu wengi nchini Afrika yakusini walimlaumu kwa picha hiyo.


Carter alikimbilia kuichukuapicha na kusahau kuwapamoja na yeye kuwamwanahabari lakini pia
alikiwa na jukumu la kuokoauhai wa binti huyu namwishoni kuacha mtoto aliwe huku yeye akishuhudia

Ndugu zangu, pamoja na kazi zetu tufanyazo tunatakiwa kufikia kipindi na kuwa na roho za utu na kuheshimu na kuwapenda binadamu wenzetu.
Kila unyama mtu unaoufanya sasa kwa binadamu mwenzako kumbuka mateso yake ni kukosa amani na mwishowe hata kujikuta ukiyachukua maamuzi kama ya Carter.
Hebu kumbuka katika maisha yako umefanya mangapi kwa makusudi na kuhatarisha maisha ya mwenzako?

Je unatambua kuwa kilabinadamu ana haki ya kuishina wewe ukiwa mmoja wapo
na kusaidia mwenzako aishi?Mungu atupe mioyo yaupendo na kuwajali wenzetu

tukiamini ya kuwa tunafuraha hivi kwa kuwa tunawaona binadamu wenzetu na kama wasipokuwepo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa maisha yetu hayana maana.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.