Friday, March 28, 2014

HISTORIA YA MMILIKI WA WhatsAppNA JINSI INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUKOSA AJIRA MUDA MREFU.



Habari za leo ndugu mfuatiliaji wa blog hii ,natumaini ni mzima wa afya ,mungu anaendelea kutupigania kila siku.Siku ya leo nataka kuwa pa moyo kwa wale ambao wanatafuta kazi muda mrefu bila mafanikio,kila unapopeleka maombi ya kazi unakataliwa,naujua uchungu huu unaokutana nao, hasa kila mwanachuo anakuwa na malengo makubwa baada ya kumaliza chuo pale anapotegemea atapata ajira muda sio mrefu,ndugu msomaji kukosa ajira kunaumiza sana kuliko kawaida ,mimi nilitafuta ajira miaka miwili bila mafanikio yoyote iliniathiri sana kisaikolojia vyote nilivyokuwa nafanya kujikimu na maisha viligonga mwamba,kwa hiyo najua uchungu wa maisha anaopitia mtu anapokuwa anatafuta ajira kwa muda mrefu.


Najua wengi wetu sasa tunatumia mtandao wa WhatsApp katika kuwasiliana,asilimia kubwa ya vijana tumejiunga humo,lakini kuna historia kubwa ya mmiliki wa WhatsAppbwana JAN KOUM ,kabla ya mwaka 2009 bwana JAN KOUM alikuwa anapenda sana maswala ya Technolojia ,kwa mara ya kwanza akasikia kuhusu kampuni  ya FACEBOOK,na kwa sababu yeye alikuwa na utalaamu wa maswala ya compyuta akaamua kwenda  kuomba kazi katika kampuni ya facebook lakini maombi yake ya kazi alikataliwa. Na hapo kabla alikuwa ameshazunguka sana kuomba kazi lakini alikuwa akikataliwa kila anapopeleka maombi ya kazi mwishoni akakataliwa kuajiriwa katika kampuni ya FACEBOOK.
JAN KOUM MMILIKIWA WHATSAPP

Baada ya kukataliwa kwenye kampuni ya Facebook bwana JAN KOUM akaamua kuacha kabisa kuomba kazi tena kwenye maisha yake ,na akaapa kabisa haji kuomba kazi tena kwenye maisha yake yote yaliyosalia hapa duniani. .Akaamua rasmi kuanzisha kampuni yake ya technolojia .Alifikira kuanzisha App  ambayo itakuwaa inawawezesha watu kutumiaa  mesegi  picha ,video na audio kwa njia ya simu,kwa hiyo akaanza kufanyia kazi wazo lake na rafiki wake wa karibu bwana Brian Acton ambaye naye alikuwa amekatiliwa maombi yake ya kazi ya kufanya kazi katika kampuni ya FACEBOOK.
JAN KOUM NA BRIAN ACTION WAMILIKI WA WHATSAPP

Baada ya kazi ngumu ya muda mrefu ya usiku na mchana na hawakuwa na fedha  mwisho wa siku  wakatengeneza WhatsApp ndio mwanzo wa kuzaliwa mtandao wa  WhatsApp. Whatsapp ilikua kwa kasi ya ajabu mpaka kufikia mwaka 2013 ilikuwa na watumiaji milioni 400 dunia nzima,ambayo ilikuwa nusu ya watumiaji wa FACEBOOK.

Mwaka jana mwishoni Facebook iliamua kununua WhatsApp kwa dola za kimarekani  bilioni 19 na zaidi hela ambayo kwa tanzania sidhani kama inahesabika ,chukua bilion 19 zidisha mara 1600 utapata jibu,mimi nimeshindwa.Ndani ya usiku mmoja JAN KOUM na BRIAN ACTION wakawa mabilionea  kutoka kwenye kampuni ya FACEBOOK ambayo mwanzoni ilikataa kuwapa ajira .


NINI TUNAJIFUNZA KUTOKA NA HISTORIA YA JAN KOUM KUWEZA KUKABILIANA NATATIZO LA KUKOSA AJIRA MUDA MREFU

1.     HAIJALISHI UNAWAZO DOGO KIASI GANI BALI KWA WAZO HILO HILO DOGO UNAWEZA KUFANYA MAKUBWA
Facebook imewalazimu kuwalipa kina Jan dola bilion 19 kwa watu ambao mwanzoni iliwaona hawafai hata kuwajiri ,lakini mwishoni imeingia gharama kubwa kwa kuhofia kampuni  WHATSAPP itawaharibia soko,hivyo hivyo wewe unayetafuta ajira kwa muda mrefu sasa kaa chini fanyia kazi mawazo yako uliyonayo kuhusu kujikwamua usijidharau wala kudharau mawazo yako na kuona hayatakufikisha popote pale,chukua hatua, sana muombe mungu songe mbele na idea ulizonazo ,mungu atafanya njia tu ,wewe tumia uwezo wako asilimia 100 ,bill gate aliwahi  kusema "tafuta wazo la kawaida lakini lifanyie kazi kwa bidii isiyo ya kawaida"

2.     KUKATALIWA NA WATALAAMU KUSIKUVUNJE MOYO
Story hii inafanana moja  kwa moja na mmiliki wa HONDA baada ya kukataliwa na kampuni ya TOYOTA na baadae kuja kuanzisha kampuni ya HONDA na kuwa mshindani mkubwa wa TOYOTA.Mameneja Waajiri wasikuvunje moyo kutokana na kukukataa kukupa ajira  na kujiona hufai,usivunjike moyo kuwa na imani na jiamini unaweza kufanya mambo mengine kwa kiwango kikubwa na kuweza kuyakabili maisha yako.Pambana sasa weka akilini mwako wewe ni mtu wa kushinda tu haijalishi unapita kipindi gani.

Naomba niishe hapa muda kwangu umekuwa tatizo kubwa kutokana na kuwa na mambo mengi ,nisiandike sana lakini na imani historia hii imekufundisha kitu kwenye maisha yako hasa kwa wewe unayetafuta ajira hivi sasa  ,historia hii pia nahakika imekupa moyo mno wa kusonga mbele,mimi pia huwa naisoma mara kwa mara maana inanipa kasi zaidi ya kutafuta mafanikio na kufika ninapotaka kufika.


Tembelea blog hii mara kwa mara naamini kila utakapoitembela kunakitu utajifunza na pia itakutia moyo katika kupamabana na maisha

Wako faraja mmasa a.k.a MOA

* SELF FULFILLING PROPHECY*

************Tafuta mafanikio kama utaishi milele lakini kumbuka kumcha mungu wako na kutenda mema kama leo ndio siku yako ya mwisho kuwepo katika dunia hii*****************************
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.