Mwaka uliopita niliandika makala kuhusu wasomi kujifunza
kujiajiri nilikusudia kuwasilisha ujumbe mmoja ya kwamba, “Wasomi na watanzania
kwa ujumla wetu tunatakiwa kubadilisha mitazamo yetu ili kujipatia mipenyo ya
kiuchumi na kifedha (financial freedom.
Kimsingi ni kwamba zipo imani zinazosapoti watu kuwa na fedha
za kutosha na zipo imani na mitazamo inayozuia watu kuwa na fedha ama
inawafanya waishi maisha ya kupungukiwa nyakati zote! Imani na mitazamo hii
kimsingi huzalishwa kutokana na malezi, utamaduni na mazingira. Mtazamo wa mtu
kuhusu fedha tunaita, “Money blue print” .
Nafahamu kuwa wengi kama sio wote tunakubaliana kuwa fedha
zina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya mtu, na kwamba ukosefu wa fedha ndio
msingi wa maovu(Ingawa wapo watu wanatumia fedha kufanya uovu wao)
tunachotofautiana ni imani kuhusu fedha. Mitazamo kuhusu fedha ndio inayoamua
kiwango cha fedha alichonacho kila mmoja. Hii ina maana kuwa kila mtu anamiliki
kiwango cha pesa sawa sawa na imani ama mtazamo wake kuhusu fedha.
vitunguu
Miaka michache iliyopita wakulima walikuwa ni watu
wanaotazamwa kama watu wenye shida, walio jitokeza kuwekeza kwenye kilimo
walionekana wameshindwa shule ( waliokimbia umande). Na hii ilisababishwa na
imani ama mapokeo ya tuliyolishwa na wazazi wetu na walimu wetu kutoka kwenye
kipindi cha zama za viwanda (Industria Age). Lakini kwa sasa dunia imebadilika
sana, kilimo kimewafikisha watu kwenye ndoto zao, Nimesoma kwenye jarida la
Forbes kwamba tajiri wa kwanza Afrika amewekeza kwenye kilimo, wajarisiamali wakubwa
hapa Tanzania wamewekeza kwenye kilimo, na wale wanaojiona wameenda shule
‘middle class’ wanaendelea kushangaa na kuendelea kuongea sentensi hasi na
kulalamikia viwango vidogo vya mishahara.
Miaka ya hivi
karibuni kwenye Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa, Mbeya,Tanga, Singida na
Kilimanjaro zao la vitunguu limejizolea umaarufu mkubwa kwa kuendelea kuajiri
maelfu ya Watanzania. Kuna ambao wamefikia ndoto zao kupitia kilomo cha
vitunguu, wamejenga nyumba, wamefungua makampuni yao, wanasomesha watoto nk.
Vitunguu hivi hivi kuna rafiki zangu wamenunua magari ya ndoto zao, wamejipa
likizo nchi za nje.