Monday, April 28, 2014

NJIA YA KUWEKA AKIBA NA KUONGEZA MTAJI KATIKA BIASHARA YAKO



Moja ya nguzo za mafanikio ya wajasiriamali ni elimu, ikwemo ya kuwaongezea upeo wa kutafuta mitaji.
Ni ijumaa nyingine tunapokutana tena katika kona hii ya mjasiriamali, hii ni kona ambayo maudhui yake ni kuona namna bora ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuanzisha na baadae kuendeleza biashara zao na kupata mafanikio wanayotamani.

Makala iliyopita ilijadili juu ya umuhimu wa kuweka akiba ili kujikinga na majanga.

Kuna msemo unasema akiba haiozi, mjasirimali unapaswa wakati wote kukumbuka msemo huu ili uwe chachu ya wewe kujiwekea akiba kwa malengo mbalimbali.

Ukiwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kutokana na mapato yako unayoyapata utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kukabilina na majanga mbalimbali ambayo yanaweza kutokea katika biashara yako, kumbuka una nafasi ya kubadilika na kujipanga upya.

Leo katika kona ya mjasiriamali tutakumbushana juu ya baadhi ya njia ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kuweza kuongeza mitaji ya biashara zao. Katika njia mbalimbali za kuongeza mitaji zipo zinazoweza kusaidia na nyingine kuumiza.

Mitaji ya biashara ni kilio cha wengi aidha kwa wale walio katika ujasiriamali au kwa wale wenye nia ya kuingia kwenye ujasiriamali. Wengi hulia kwamba watapata wapi mtaji kwaajili ya kuanzisha biashara au kwaajili ya kuendeleza biashara.

Wajasiriamali wanapaswa waelewe kwamba kuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza mtaji katika biashara wanazofanya. Muhimu zaidi ni kufahamu njia hizi ili kuweza kuangali ni ipi kwa hatua uliyofikia inaweza kukusaidia zaidi badala ya kukuumiza.

Yafaa pia kujiuliza je ni sababu zipi zinazopelekea wewe kuwa na hitaji la ongezeko la mtaji katika biashara yako  na nini matokeo tarajiwa. Kujiuliza maswali haya na mengine itakusaidi kufanya uamuzi sahii. Zifuatazo ni njia za kuongeza mitaji ya biashara yako.

Njia ya kwanza ni uwekaji wa akiba. Uwekaji wa akiba ni njia ya kwanza ambayo inaweza kukusaidia katika kukuza mtaji wako wa biashara. Kma utakuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ni rahisi kwako kutumia akiba ili uweze kukuza mtaji wako.

Iwe kwa mjasiriamali mwenye biashara mpya au inayoendelea ni muhimu sana kufikiria kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara. Uwekaji wa akiba ni moja ya njia ya kukuza  mtaji ambayo haina gharama wala matatizo kuliko nyingine yoyote.

Uwekaji wa akiba ni njia inayoonekana ngumu kati ya watu kwasababu ni njia ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu. Unapotaka kutumia njia hii ili kuweza kukuza mtaji wa biashara au kuendeleza biashara unahitaji nidhamu katika matumizi ya fedha zako.

Jiulize je matumizi ya fedha zako yakoje? Ni yapi yamekuwa matumizi ya msingi na yapi si ya msingi, kwanini usipunguze au kuacha matumizi yasio ya msingi na kuweka akiba ili kuweza kukuza mtaji kwaajili ya biashara yako.

Jiulize unatumia kiasi gani cha fedha zako kwaajili ya ‘vocha’, unatumia kiasi gani kwaajili ya pombe, unatumia kiasi gani kwaajili ya starehe, vipi michango ya harusi, je unatumia kiasi gani kwaajili ya burudani nyingine ambazo si za msingi!

Kaa chini na utafakari juu ya mapato na matumizi yako na angalia ni kwa namna gani unaweza kuweka sehemu ya mapato yako kama akiba kwaajili ya aidha kukuza mtaji wa biashara unayofanya au kuanzisha biashara mpya na malengo mengine ya baadae.
Share:

MAMBO KUMI YA MSINGI YA KUFUATILIA UNAPOKUWA UNAJIANDAA NA MITIHANI



Habari za leo mfuatiliaji wa blog hii ya Faraja Mmasa Blog, natuamini ni mzima wa afya njema maana mungu wetu mpendwa anatupigania kila sekunde.Asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mara kwa mara wa blog hii lakini pia nikupongeze kwa kuwa mfuatiaji wa mara kwa mara kwa kuwa kila unapoingia katika blog hii basi kuna kitu kipya unajifunza kila siku katikachokusaidia katika maisha yako ya  kila siku.Mada  ninayotaka kuilezea leo inahusu hasa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda kujiandaa na mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita,Mimi ninawaombea sana kwa mwenyezi mungu kila mmoja akafanye mitihani kwa utulivu na kuweza kusonga mbele, nimeinadika mada hii kwa ajili ya wanafunzi wote wa kidato cha sita lakini pia na mimi pia mdogo wangu kipenzi wa mwisho Jackline Kaboko anajiandaa kufanya mtihani huo,kwa hio nikaona sio vyema kukaa na kumuelezea nini cha kufanya peke yake basi ,bali niongee na wanafunzi wote wanaojiandaa na mtihani huu.Mada hii pia nitaifundisha katika Redio ya Sibuka 94.5 fm siku ya jumatatu na alhamisi kuanzia  saa tisa na dakika 20,hivyo basi pia unaweza kunisikiliza kupitia Radio.
Share:

KUHUSU MMILIKI WA BLOG HII

My photo
Naitwa faraja Mmasa a.k.a Moa,Mkazi na mzaliwa wa Wilaya ya Gairo Morogoro.KARIBU KATIKA BLOG hii tuelimishane mambo mbalimbali.Inatupasa kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ili tuweze kuyatawala Mazingira yetu .Kuwa na Mwanasheria au Mhasibu haimanishi unatikiwa kujua au kufuatilia maswala ya uhasibu na sheria tu.Mfano nyumba yako au ndoa yako hutaindesha kwa taaluma uliyonayo.Vile vile huwezi kuendesha ujasiliamali kwa mafanikio kwa shahada yako ya uhandisi.TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

UJUMBE WA LEO

MIUJIZA MINGI INAYOTOKEA KATIKA MAISHA IPO KATIKA MAWAZO,FIKRA,NA IMANI ALIYONAYO MWANADAMU HUSIKA

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

USIKOSE KIPINDI HOT JIJINI POWER CLUB ,SIBUKA REDIO 94.5 KILA SIKU SAA SABA MPAKA SAA KUMI

GAR AD2

GAR AD2

GARI ADVERT

GARI ADVERT

Castrol

Castrol
Powered by Blogger.